Fahamu Gharama Katika Kilimo cha Nyanya

Hapa nitaelezea, kujulisha, kuainisha, na kudadavuwa juu ya gharama za kilimo cha nyanya kwa uchache Zaidi

kulingana na utofauti wa kikanda na mazingira, nitajulisha gharama za manejimenti ya shamba pekee; yaani gharama za mbegu, madawa na mbolea zinazohitajika kwenye shamba la nyanya kuanzia mwanzo hadi mavuno.Gharama za kodi ya shamba, umwagiliaji, wafanyakazi na miundombinu ya shambani haitoainishwa kulingana na kutofautiana kwa gharama hizi kulingana na eneo au ukanda husika.
Gharama hizi zitakuwa kwa eneo la ekari moja pekeeHii itasaidia mkulima kufahamu, kujuwa na kupanga bajeti ya ujumla kabla ya kuanza mradi wa kilimo cha nyanya.
Ikumbukwe kuwa; zao la nyanya shambani ni Zaidi ya mtoto mchanga katika malezi na matunzo; zao la nyanya linahitaji umakini mkubwa sana katika kipindi chote cha ukuwaji mpaka hadi mavuno. Maana hii ni kwamba; Smkulima anapaswa kutembelea na kujuwa hali na maendeleo ya ukuwaji wa shamba kila siku.

MABEGU BORA ZA NYANYA NA GHARAMA ZAKE

JINA LA MBEGU KIASI KWA EKARI BEI YA MBEGU
AINA MSIMU/HALI YA HEWA
COMMANDO F1 30-40 gm 240000 MSHUMAA BARIDI/MVUWA NYINGI
SIFA F1 30 gm 330000 MSHUMAA JOTO/ MVUWA CHACHE
RANGER F1  30 gm 330000 MSHUMAA JOTO,MNYAUKO, BARIDI, MVUWA NYINGI
SIFA F1 30 gm
MSHUMAA MAZINGIRA YOTE




MADAWA YA UKUNGU NA GHARAMA ZAKE KWA EKARI MOJWAmadawa ya kudhibiti magonjwa ya fangasi/ukungu/barafu/kuvu hupaswa kupigwa mara zaidi shambani kuliko madawa ya wadudu.
mkulima anapaswa kupiga madawa ya fangasi kila baada ya siku 7 hadi 14, kulinagana na ahali aya hewa.
kwa kipindi cha mvuwa nyingi; mkulima atapaswa kupiga dawa kila baada ya siku 7. ni vyema kupiga dawa ya kukinga au kutibu na kukinga kabla ugonjwa haujaonekana au kutokea.
kwa mantiki hiyo ni kwamba waweza tumia dawa yeyote kati ya hizi zilizoorodheshwa chini kwa kukinga.
na kama ugonjwa umekwisha ingia; itabidi upige dawa ya kukinga na kutibu.

GHARAMA ZA MADAWA YA WADUDU.
Wadudu wasumbufu Zaidi kwenye zao la nyanya namba moja ni KANITANGAZE, ikifuatiwa na vipepeo weupe, vimamba, leaf miners n.kWadudu hawa hudhibitiwa vizuri Zaidi kwa kupiga dawa mchanganyiko wa dudumectin au wilcron na wiltigo plus.Wiltigo plus inauwezo mkubwa Zaidi wa kumdhibiti kanitangaze kwani hutoa kinga ya muda mrefu Zaidi (siku 21).Hivyo ninawashauri wakulima kutumia Amsac, Liberity, belt, Couragen kuanzia mara tu utakapopandikiza miche shambani mpaka hadi mavuno.

Changanya kiasi cha 5 mls wiltigo plus na 30 mls dudumectin au wilcron katika lita 16 hadi 20 za maji.
Kumbuka kupiga dawa ya wiltigo plus kila baada ya siku 14-21 ili kuweka kinga dhidi ya kanitangaze,mdudu hatari Zaidi kwa zao la nyanya.

GHARAMA ZA MBOLEA KATIKA ZAO LA NYANYA.

MUDA BAADA YA KUPANDIKIZA MBOLEA KIASI KWA EKARI GHARAMA
WIKI 1-2 DAP (bora) 50 Kg 66,000- 67,000
YARAMILA OTESHA (bora Zaidi) 50 Kg 63,000-65,000
YARAMILA WINNER 50 Kg 65,000 – 68,000
WIKI 3-4 YARAMILA WINNER (bora Zaidi) 50 Kg 65,000 – 68,000
YARAVERA AMIDAS 50 kg 57,000 -58,000
UREA 50 Kg 56,000
NPK (bora) 50 Kg 59,000-61,000/=
MAUWA YA KIKARIBIA KUTOKA YARALIVA NITRABOR (bora Zaidi) 50 kg 70,000-74,000/=
CAN 50 kg 43,000-45,000/=
MATUNDA YAKITOKA YARALIVA NITRABOR+ NPK/ WINNER 25 Kg : 50 kg 35,000 + 59,000/68,000/=
BAADA YA MCHUMO WA KWANZA YARALIVA NITRABOR+ NPK/ WINNER 25 Kg : 50 kg 35,000 + 59,000/68,000/=

MAELEZO: katika orodha tajwa ya mbolea hapo juu, mbolea zote ni bora Zaidi kutumika .NB: mbolea ya samadi haijainishwa kutokana na utofauti wa gharama kulingana na eneo.Ni bora Zaidi kutumia mbolea ya samadi kabla ya kupandikiza miche shambani.Hivyo kwa Makala hii gharzima mkulima ataamuwa atumie mbegu ipi, dawa zipi, na mbolea zipi kwa ghaarama ipi ili kufanikisha mradi mzima wa kilimo cha nyanya.

The post Fahamu Gharama Katika Kilimo cha Nyanya appeared first on Kilimo Tanzania.